Haya ni mambo 14 yatakamfanya mwenzi wako afurahie kurudi nyumbani pindi siku yake itakapoisha akiwa kazini au safarini.
- Salamu ya itakayomfurahisha kwa kufurahiwa na mpenzi wake
2. Hamu ya kufahamu na kukufahamisha siku yake ilikuwaje?
3. Sehemu yenye amani na uhakika kwamba mwenza wake ndiye atakayempatia amani hiyo.
4. Tabasamu lako na vicheko. Siku imeshakua ngumu nje tayari mrahisishie afikapo nyumbani.
5. Uthibitisho wa mapenzi yako.
6. Japo busu kutoka kwako (kumbuka mlipigana mabusu mengi sana wakati wa mahusiano yenu na mwanzo wa ndoa) .
7. Nafasi ya kupata chakula cha usiku na wewe na watoto kama mnao.
8. Ujumbe mfupi kutoka kwako kama anajisikia vibaya au anamaumivu yoyote.
9. Maneno ya kuhamasisha endapo alikuwa na siku mbaya.
10. Maneno yenye kutoa sifa na kuonyesha husuda kwa mwenzi wako.
11. Kufunga siku kwa matumaini na mategemeo ya kesho kuwa nzuri kwenu nyote.
12. Muda wa faragha na wewe chumbani.
13. Kufanya mapenzi na wewe endapo wote mko na hitaji hilo.
14. Aidha busu, kumbato au sala ili muweze kulala salama na akwa amani.
Chapisha Maoni