Mwanamke mmoja nchini Vietnam amezua gumzo baada ya kujifungua watoto mapacha ambao kila mmoja ana baba yake. Hali hii imezua tafarani baadhi ya watu kuhoji inawezekana vipi mzazi kuwa na watoto mapacha ambao si wa baba mmoja?
Mtaalamu wa masuala ya uzazi nchini humo ameelezea ni kivipi hali hii inaweza kutokea na kusema kuwa,
Watoto mapacha wenye baba tofauti wanaweza kutokea endapo mwanamke atafanya mapenzi na wanaume wawili tofauti kati ya siku moja hadi saba za kupevuka kwa yai.
Mwanamke anaweza kupevusha mayai mawili kwa mwezi huo ambapo moja litarutubishwa na mbegu za mwanaume mmoja na jingine kurutubishwa na mbegu za mwanaume wa pili. Mbegu za mwanaume zinauwezo wa kuishi takribani saa 72 hivyo mayai hayo yanaweza kurutubishwa siku tofauti.
Chapisha Maoni