Meli ya mizigo ya MV Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam alfajiri ya jana ilizama kabla ya kufika Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa imebeba mizigo inaelezwa na Kapteni wake kuwa ilitoboka pampu na kuanza kuingiza maji ndani hivyo alijitahidi kuipeleka ufukweni mwa bahari ili kuizuia isizame katikati ya bahari.
Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyezama na kupoteza maisha, kwa mujibu wa mashuda wa ajali hiyo meli hiyo imetoboka na kupitisha maji na ikabidi mabaharia wa meli hiyo kutosa baadhi ya mizigo bahari kuokoa maisha yao na kufanikiwa kufika katika eneo hilo.
Video ikionyesha zoezi la uopoaji wa mizigo kutoka katika meli hiyo.

Askari wa FFU wakiwa katika ufukwe wa pwani hiyo kilinda mizigo inayoopolewa katika Meli hiyo ili kuwa katika hali ya usalama kuepusha vibaka kuiba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud na Wananchi wakiwa katika ufukwe wa pwabni ya kilimani wakati wa kuokolewa kwa mizigo ya mali hiyo na kufikishwa katika eneo hilo kwa kuhifadhiwa na kuchukuliwa na wenye mali zao.
Baadhi ya magunia ya mbatata na vitunguu yakiwa wameokolewa katika meli hiyo na kufikishwa nchi kavu katika pwani ya kilimani Zanzibar.
Baadhi ya Mbao zilizookolewa katika meli hiyo zikiwa nji kavu baada ya kuokolewa katika meli hiyo.
Ubuyu ukiwa umeharibika kutokana na ajali hiyo ya kuzama kwa meli hiyo baada ya kuingia maji baada ya kupata hitilafu ya kutoboka na kuingia maji ndani.
Boti za wavuvi zikiokoa mali katika meli hiyo na kuzivikisha ufukweni mwa bahari ya kilimani Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika ufukwe wa pwani ya kilimani akiangali meli hiyo wakati wa kuokoa mezigo iliokuwemo katika meli hiyo ikitokea Dar es Salaam ikiwa na mizigo ya wafanyabiashara wa Zanzibar.
Wachukuzi wakibeba magunia ya mbatata baada ya kufikishwa ufukweni na boti zilizokwenda kupakia mizigo hiyo katika meli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo la kuzama kwa meli hiyo wakati alipofika katika eneo la tukio leo asubuhi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ajali hiyo na kusema Maofisa wake wa Idara ya maafa Zanzibar wanafuatilia ajali hiyo na kutowa msaada na kutowa pole kwa mabaharia wa meli hiyo kwa ajili iliyowapata na kuwafariji wafanya biashara kwa asara waliopata kutokana na kupotea kwa bidhaa zao.
Mfanyabiashara wa Zanzibar ambae bidhaa zake zilikuwemo katika meli hiyo akizungumza na waandishi wa habari kutokana na ajali hiyo na kupata hasara kwa kupotea kwa bidhaa zake na baadhi ya nyengine kuharibika kwa kurowa kwa maji ya chumvi.
                                                                                        
Share this