Yapata miezi miwili sasa tangu tuzisikie taarifa za
msanii mkali kutoka Nigeria
Davido kutoa malalamiko kwa uongozi wa lebo ambayo inasimamia kazi zake kwasasa
#Sony Music.
Malalamiko hayo yalitokana na kilichosemekana kuwa
uongozi huo unamzuia msanii Davido kuachia kazi mpya bila kujali kuwa ni
kipindi kirefu kimepita kwa msanii huyo bila kutoa kazi mpya.
Kutoka Bongo Flevani msanii @officialalikiba naye
pia yupo chini ya uongozi huo wa Sony Music. Ila yeye ameiambia Perfect255 kuwa
jambo kama lile lililomtokea Davido yeye
haliwezi kumkuta kutokana na mkataba wake ambao amesaini na kampuni hiyo.
Ni baada ya kuulizwa kuwa yeye amejipanga vipi
kama endapo litatokea kama lililomtokea msanii
mwenzake Davido katika lebo hiyo. “Nimejiandaa vizuri, na pindi unapokuwa
unasaini kitu ina maana kuwa umekubaliana na kila kitu, kwahiyo mimi pia nina
matakwa yangu na hata wao pia wana matakwa yao, kwahiyo kitu ambacho kipo hapo
ni kwenda na agreement. Me siwezi kukaa muda zaidi ya miezi 3 bila kutoa ngoma,
na huo ndio mkataba wangu jinsi unavyosema.” Hayo ndio yalikuwa majibu ya
Aikiba.
Filed Under:
WASANII
Ijumaa, 4 Novemba 2016
Chapisha Maoni