1. Serikali yatoa msimamo mapenzi ya jinsia moja
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, amesema mapenzi ya jinsia moaja hayakubaliki na Serikali ilishaweka msimamo wake akatika hilo. Alisema hayo jana katika mkutano na wadau wa haki za binadamu uliofanyika jijini Dar es salaam, kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuweka mikakati ya kuishawishi Serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa – Nipashe
2. Askari wa FFU ahukumiwa kwenda Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mwanafunzi
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Raphael Makongojo (25) aliyembaka mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Pia Makongojo amepewa adhabu kali, ikiwemo viboko 12 pamoja na kuamriwa kutoa faini ya Sh milioni 15 mara atakapomaliza kifungo chake – Habari Leo
  1. Serikali mbioni kuruhusu matangazo ya Bunge ‘live’ redioni
Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kuviruhusu vituo vya redio nchini, kurusha matangazo ya vikao vya Bunge moja kwa moja. Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupokea maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo wanahabari waliokwenda Dodoma, kuonana na Uongozi wa Bunge kujadili suala hilo la matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa studio ya kuzalishia vipindi ya Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA) iliyopo Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  1. Kwa atakaempa mimba mwanafunzi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela
Bunge limepitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 ya mwaka 2016 ambayo pamoja na mambo mengine, imeongeza adhabu kwa watu wanaowapa mimba au kuoa ama kuolewa na mwanafunzi, sasa watafungwa jela miaka 30. Sheria hiyo ilipitishwa jana bungeni mjini Dodoma baada ya Muswada kuwasilishwa Juni 24, mwaka huu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambao baadhi ya wabunge walipata fursa ya kuuchangia. Muswada huo ulilenga kufanya marekebisho katika sheria 21 kwa lengo la kuondoa mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo na umepitishwa kuwa sharia – Mtanzania
  1. Maonyesho ya sabasaba yaanza leo rasmi.
 Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanaanza leo yakishirikisha nchi 30 na kampuni za ndani na nje ya nchi 2,500 zimethibitisha kushiriki. Licha ya kuwapo kwa idadi hiyo iliyothibitisha kushiriki maonesho hayo yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi Julai mosi mwaka huu na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, bado washiriki wengi hawajakamilisha maandalizi katika mabanda yao. Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Anna Bulondo alisema, hadi jana mchana kampuni 2,000 za ndani na 500 kutoka nchi 30 zimejiandikisha kushiriki na kupewa maeneo ya kuonesha bidhaa na huduma zao – Habari Leo
  1. Mechi ya Yanga vs TP Mazembe.
 Baada ya mashabiki wa Yanga kutangaziwa kwamba Mechi hiyo leo itakua bure, watu walianza kuingia Uwanjani humo tangu saa mbili asubuhi, na mpaka kufikia saa nane uwanja wa Taifa ulikua umeshajaa na mageti kufungwa. Wakati huo huo kuna mashabiki wengine walioshindwa kuingia ndani ya uwanja huo walianza kusukuma mageti na kulazimisha kuingia ndani na ndipo polisi walipoamua kurusha mambomu ya machozi kutuliza vurugu zilizozuka nje ya uwanja huo. Mchezo umekwisha kwa TP Mazembe kuibuka na ushindi wa bao 1-0
  1. Tundu Lissu apandishwa kizimbani Kisutu kwa uchochezi.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amepandishwa kizimbani baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kujibu tuhuma za kuchapisha chapisho la uchochezi lenye kichwa cha habari’ Machafuko yaja Zanzibar’. Lissu alifika mahakamani hapo jana saa tano asubuhi, kwa ajili ya kuitikia wito wa kumtaka kwenda kujibu tuhuma za uchochezi zinazomkabili baada ya washitakiwa wenzake wawili akiwemo Mhariri wa Mawio ambalo lilifungiwa kwa muda usiojulikana, Simon Mkina kusomewa mashitaka. Mbunge huyo na washitakiwa wenzake Mkina na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
  1. Kesi ya David Mwangosi kutolewa hukumu mnamo Julai 21, 2016
Mahakama kuu kanda ya Iringa inaendelea na vikao vya kusikiliza kesi ya mauaji ya mwanahabari mkoani mkoani humo, Marehemu Daud Mwangosi, inayomkabili mtuhumu wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573. Aidha mahakama hiyo imetaja tarehe 21 mwezi wa 7 mwaka huu kuwa ndio siku ya kutoa hukumu ya keshi hiyo. Taarifa zinaeleza kuwa endapo mtuhumiwa wa mauaji ya Daudi Mwangosi atapatikana na hatia ya kutenda kosa hilo basi atahukumiwa kunyongwa hadi kufa.